-----------------------------------
BINAFSI
-----------------------------------
OGOPA watu wakimya. Ni rahisi watu kama hawa kufurahi kama ilivyo katika kukasirika. Na wanapofurahi hudhihirisha hili. Wanapokasirika hulizuia kwa ndani. Na wao kupasuka kama bomu ni kitu cha kawaida. Kama una mtu wa nanmna hii yapaswa uwe karibu naye sana.
------------------------------
NYUMBANI-------------------------------
NYUMBA kwa wengi wetu sio zaidi ya chumba cha kulala na choo. Ni nadra sana kwa baadhi yetu kuona hali katika maeneo mengine ya nyumba. Jenga tabia ya kukimbia chumba na choo chako ili uone wanao chini ya paa lako wanaishi vipi.
--------------------------------
NJIANI---------------------------------
NJIANI sio mahala pa makelele labda katika hali isiyo ya kawaida. Watu na jamii iliyostaarabika huonekana sio katika majumba yao tu bali pia wanavyochanganyika na watu wengine. Mtu mstaarabu kwa ndani anaweza akawa mshenzi wa mwisho barabarani.
--------------------------------
SAFARINI--------------------------------
KUNA vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kuwa navyo unapokuwa safarini. Kwa mfano, sindano ya kushonea nguo na vifungo, Vingine ni chana, brashi ya viatu na nguo. Aidha mswaki, dawa ya mswaki, sabuni na marashi. Muhimu zaidi hata hivyo ni dawa zinazokusaidia mara kwa mara, kama zile za malaria, kichwa na kuzuia kuharisha na kutapika.
---------------------------------
SHULENI-----------------------------------
FANI ya uigizaji na maigizo katika shule nyingi za msingi imekufa. Katika miaka hii ambayo nchi sasa ina televisheni na inatengeneza sinema ni muhimu kuirudisha fani hiyo kwa nguvu mpya. Hili sio lazima lingojee serikali. Shule na idara za serikali, sekta ya umma na sekta binafsi zinaweza kulifufua kwa faida ya kurahisisha kazi na biashara za wote.
---------------------------------
KAZINI-----------------------------------
KAZI inayokuweka mahala pamoja tu haiwezi kukupatia mshahara na maslahi mazuri. Ukitaka ufaidi kazi lazima uwe na kazi yenye safari mzomzo. Kwazo hizo utaweza kuweka mshahara wakao kama akiba na kuufanyia zaidi kazi za maendeleo badala ya kuwa ni tonge la mkono kwenda kinywani tu.
----------------------------------
NCHI ZA NJE----------------------------------
ITAKUWA ni kupunguza kwa kiasi kikubwa kwa balozi za Tanzania nchi za nje kujenga au kununua hosteli na kuzipendezesha zifanane fanane na hoteli za kitalii. Hosteli hizo zikiwepo Watanzania waendao nchi hizo watakuwa na mahala nafuu na salama zaidi kulala. Na siyo tu hayo bali watakuwa wanapata huduma muhimu pamoja na ushauri wa shule, biashara na uwekezaji palepale ubalozini.
-----------------------------------
BURUDANI----------------------------------
MICHEZO ya kuigiza ni burudani moja ya aina yake. Wakiwepo watunzi wa hadithi na waigizaji wazuri mchezo wa kuigiza unaweza kuwa ni starehe na wakati huo huo darasa juu ya jambo muhimu katika maisha au katika suala la uchumi, siasa na utamaduni wa jamii husika. Tufufueni michezo ya kuigiza kwa kwenda mbele.
----------------------------------
MICHEZONI----------------------------------
MICHEZO bila washangiliaji sio mchezo. Na watu wachache kwa tamaa zao wanaweza kupandisha viingilio kiasi visilingane na thamani ya fedha apatayo mteja lakini hili siku moja litawatumbukia nyongo.
Lazima pawepo na njia za kisayansi za kukadiria nini iwe kiingilio cha kuingia katika shughuli fulani. Vinginevyo ni wizi!
-----------------------------------
MJINI-------------------------------------
MJINI ni mahala pa biashara. Na wafanyabiashara wengi ni wapangaji wa nyumba za watu wengine. Na inajulikana jinsi mpangaji au wapangaji fulani wanavyoweza kuzozana na mwenye nyumba. Wakifukuzwa wakaja wengine, je, ipo haki kwa shirika kama TANESCO kuwanyima umeme wapangaji wapya au TANESCO haijui biashara na inaendelea kuomba ruzuku tu toka serikalini ?
-------------------------------------
VIJIJINI-------------------------------------
KUNA vijiji ambavyo havistahili kuwa na tatizo la kukosa chakula kwa kuwa kuna mifereji ya maji ya kunyweshea mashamba. Kazi ni kutunza na kuendeleza mifumo hiyo ya umwagiliaji kwa namna isiyo na ujanja au upendeleo. Vijiji kama hivyo sio tu vitajitosheleza kwa mahitaji yao ya chakula bali pia vitauza ziada kwenye vijiji na miji mingine.
sammy.africa2100@gmail.com
Tuesday, December 1, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment